KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ATOA WITO KWA WATANZANIA WENYE VIRUSI VYA UKIMWI KUJITANGAZA HADHARANI


Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kujitangaza hadharani mara wanapopimwa na kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Wito huo umetolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu, Mtumwa Khalfan, wakati akitoa ujumbe wa mbio hizo mara baada ya Mwenge huo kuwasili Manyoni juzi na kuanza kwa siku mbili mkoani Singida.

Mtumwa alisema licha ya kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, baadhi ya watu wamekuwa wagumu kujitangaza na kusababisha wakose fursa na huduma mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo, Mtumwa alisema ni vyema wanaoishi na virusi vya UKIMWI waache kujinyanyapaa badala yake wajitangaze hadharani juu ya hali ya afya zao.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia watambulike vyema na jamii ya eneo husika na kuwa rahisi kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali na wadau wengine

Posted by Bigie on 11:22 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.