NAAKAYA AAMUA KUACHANA NA SIASA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia aliwahi kujihusisha na masuala ya siasa nchini, Nakaaya Sumari, amejutia uamuzi wake wa kugeukia siasa, akisema amepoteza muda mwingi pasipo manufaa yoyote.
Nakaaya ambaye aliwahi kushiriki katika mashindano ya kwanza ya Tusker Project Fame mwaka 2006, sasa ameamua kuachana na siasa kwa lengo la kuutumia muda wake kuelimisha jamii kupitia muziki.

“Nimegundua nilifanya maamuzi yasiyo sahihi, katika kipindi chote nilichokaa ndani ya siasa haijanisaidii chochote hivyo nimeamua kujiondoa. Nitabaki kwenye muziki tu ambako ndiko kipaji changu kilipo, alisema Nakaaya.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa “Mr Politician”, alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwaka 2009 na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, alihama na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Posted by Bigie on 7:34 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.