RAIS WA TANNZANIA AMUAPISHA BALOZI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU-DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika jana  Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Nyaraka za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Ombeni Yohana Sefue, mara baada ya kumuapisha rasmi, jana  Ikulu Dar es Salaam.
Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa ukumbini wakati akisubiri kuapishwa rasmi kushika madaraka ya Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Ikulu Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo jana  Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo jana Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika jana  Ikulu Dar es Salaam

Posted by Bigie on 11:46 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.