JAJI KHAMIS ( KASHI) AUANZA MWAKA VIZURI KWA KUVISHWA PETE YA UCHUMBA


MSANII mwenye heshima na mkongwe katika sanaa ya uigizaji Bongo, Jaji Khamis ‘Kashi’  ameuanza mwaka vizuri kwa kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa muda mrefu aliyejulikana kwa jina la Brian Sylvester.

Tukio hilo lilichukua nafasi Januari 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Sterio, Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki.

Akizungumza kwa furaha mara baada ya kidole chake cha pete ‘kupendeza,’ Kashi alisema: “Namshukuru Mungu kwa kunijaalia mwanaume kama huyu anayeelekea kutimiza ndoto zangu, nampenda, ananipenda, naamini tutadumu.”

Posted by Bigie on 2:59 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.