JINI ALILOTUPIWA IRENE UWOYA LAZIDI KUMTESA


MATATIZO ya staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya yanayomfanya asiwe mtulivu kwenye ndoa yake, yamedaiwa kuwa yanasababishwa na jini mbaya aliyetupiwa.

Jumamosi iliyopita kwenye Gazeti la Risasi, Uwoya alinukuliwa akidai kuwa anahisi kuna mtu amemroga ili amchukie mume wake, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ndiyo maana humpenda na kumkumbuka wakiwa mbali lakini wanapokuwa karibu humchukia.

Kutokana na madai hayo ya Uwoya, mganga mmoja aliyejitambulisha kuwa na elimu kubwa ya majini, Maalim Sultan Mpweza amedai kuwa ni kweli mrembo huyo amerogwa lakini siyo kwa uchawi ila ametupiwa jini.

Maalim Sultan alisema, amefuatilia kwa muda mrefu matatizo ya Uwoya na jinsi ambavyo ameshindwa kutulia kwenye ndoa na kubaini kuwa mrembo huyo hana makosa ila mtu muovu ni yule aliyemtupia jini mbaya kwa lengo la kuisambaratisha ndoa yake.

“Ametupiwa jini mbaya sana, anaitwa Brulefer. Huyu akitupiwa mwanamke hawezi kutulia kwenye ndoa. Akili yake huvurugika na huibua visa bila sababu,” alisema Maalim Sultan na kuongeza:

“Kwa hali iliyopo ni kwamba Ndikumana hamuwezi, wataendelea kugombana. Anatakiwa apate tiba kwa kutuona wataalam kama sisi au kama anashindwa kufanya hivyo, basi amuombe sana Mungu. Sala na dua mara nyingi hukimbiza majini wabaya mwilini.”

Maalim Sultan alifafanua: “Kama Irene ameanza kujitambua kuwa amerogwa, maana yake kuna nguvu imemuingia na kumzindua, kwa hiyo kazi ni kwake kutafuta tiba. Nikiangalia kitaalamu, naona ndoa ya Irene na Ndikumana ni yenye mafanikio makubwa kwa sababu mume anampenda sana mke wake na yupo tayari kumfungulia biashara.”

Uwoya na Ndikumana, walifunga ndoa Julai 2009 na kufanikiwa kupata mtoto Mei mwaka jana ambapo hivi karibuni ulitokea mzozo mkubwa uliosababisha wawili hao kutangaza kuachana.

Yapo madai kuwa Irene amekuwa si muaminifu kwenye ndoa yake, wakati huohuo inavumishwa kwamba hata mtoto si wa Ndikumana ingawa wote wanaungana kukanusha uvumi huo.

Posted by Bigie on 2:11 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.