JOHARI "AYALAANI" MAGARI.......NI BAADA YA KUNUSURIKA KUFA KWA AJALI MARA MBILI


BAADA ya kunusurika kifo mara mbili, msanii mwenye jina kubwa katika tasnia ya filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema kwa sasa hataki tena kuendesha magari,


Akizungumza na mpekuzi wetu, Johari aliweka wazi kuwa kutokana na kunusurika huko kifo, sasa hataki tena kuendesha magari  na badala yake atakuwa anamtumia dereva wake mwenye utaalamu.


Msanii huyo aliyasema hayo baada ya hivi karibuni kupata ajali ya gari iliyotokea Ubungo, Dar katika Barabara ya Mandela huku kumbukumbu zikionesha kuwa aliwahi kupata ajali ya aina hiyo katika barabara hiyohiyo siku za nyuma.


Alipoulizwa kama anafikiri ajali hiyo ina mkono wa mtu, Johari alikiri kuwa na maadui wengi ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza kuwa chanzo.


“Hebu fikiria, kwa sasa ni mara mbili napata ajali ya gari tena barabara ileile, hivyo, kwa sasa sitaki kuendesha nitamtumia dereva wangu na kama hayupo nitatumia njia nyingine lakini si kuendesha mimi,” alisema.


 Akaongeza:“Sitaki kuamini hivyo japo kweli maadui ni wengi, lakini kwa sasa hakuna usafiri ninaouchukia kama wa gari.”

Posted by Bigie on 10:39 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.