MASHAUZI CLASSIC BAND WAJIPANGA KULITEKA SOKO KWA UJIO WA ALBAM YAO MPYA


MSANII wa taarabu ambaye ni mmiliki wa bendi ya ‘Mashauzi Classic’, Isha Mashauzi, amesema kuwa wanajipaga kutoa albamu yao inayokwenda kwa jina la ‘Si bule una mapugufu’, ambayo itakuwa na nyimbo nne huku ikitarajia kuwa sokoni Aprili mwaka huu.

Alizitaja nyimbo hizo kuwa ni
‘Si bule una mapungufu’, ‘Niacheni nimpende’, ‘Fungu la kukosa’, ‘La mungu halina muamuzi’.

Isha
alisema albamu hiyo ndiyo itakayo mtambulisha yenye pamoja na bendi yake kwani anaamini itafanya vizuri kuliko nyimbo zile ambazo alikuwa anaziimba awali.

“Hiyo ndo mpya ambayo tunayo hivi sasa na tunaamini albamu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali kwani nyimbo zote zimetungwa kwa umakini wa hali ya juu,”
alisema.

Aliongeza kuwa anawashauri mashabiki wa muziki wataarabu hasa wapenzi wa
Mashauzi Classic nchini kukaa tayari kuipokea albamu hiyo kwani uzinduzi wake utakuwa baada ya kutoka ambapo ni mwezi wa nne.

Posted by Bigie on 3:22 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.