MSANII UCHE ULENDU AFUNGA PINGU ZA MAISHA...
2:18 AM
Uche Elendu amekata ngebe za wapinzani wake baada ya kufunga harusi nyeupe iliyovutia na mumewe Walter Ogochukwu Igweanyiba, mjini Owerri nchini Nigeria.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na mastaa kadhaa ingawa wanasiasa ndio waliokuwa wengi zaidi wakiongozwa na Spika wa Bunge la Nigeria.
Mume wa msanii huyo ambaye ni mfanyabiashara wa kimataifa alichafua mji huo kwa magari tofauti ya kifahari zikiwemo Benz na Jeep ambazo zimeacha gumzo.
Maswahiba wa mwanamke huyo waliokuwepo kwenye sherehe hiyo ni Rita Tony Edoche, Sophia Tchidi Chikere, Francis Duru, Oge Okoye, Emeka Onyiocha, Obot Etuk, Maureen Solomon, Adaorah Ukoh ambao wote ni wasanii






