RAY C AWAPONDA WASANII WA TANZANIA......ADAI KUWA MAJUNGU YAMETAWALA KAZI ZAO


MSANII wa muziki wa bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya kazi zake nchini Kenya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amezungumza na Mpekuzi wetu  na kusema kuwa wasanii wa bongo wanatumia ushirikina katika muziki huku wakifanya kazi hiyo kwa majungu na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ahamie nchini humo.

Ray C
aliyasema hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalum na mtandao  wetu juu ya masuala mbalimbali ya kimuziki.

Alisema kuwa yeye ni mkali lakini baadhi ya watu wanambania asifanye vizuri kwa lengo la kumpoteza katika sanaa kitu ambacho kilimlazimu afunge safari na kwenda nchini humo.


Alisema kwa muda mrefu amekuwa akitoa kazi lakini baadhi ya watu ambao ni washirikina walizilikalia zisitoke kitu ambacho kilimuumiza sana kichwa huku wengine wakitoa maneno ya mafumbo juu yake kwamba tayari ameshafulia kimuziki.


Akizungumzia muziki wa
Kenya msanii huyo alisema kuwa nyota wa nchini humo wanafanya kazi kwa kujituma na hawana majungu kama walionayo baadhi ya wasanii wa bongo.

Alisema tangu anze harakati zake za kurekodi nchini humo hakuna msanii ambaye alimuonyesha dharau kitu ambacho kinampa hamasa ya kuendelea kuishi huko kwani hadi sasa tayari amesharekodi nyimbo kadhaa ambazo bado hajazipa majina.


“Unajua mazingira ya huku mazuri kwa sababu hakuna msanii ambaye anadharau kama bongo, kwanza unafanya kazi kwa wakati yaani napenda kuishi huku kutokana na vitu hivyo,”
alisema.

Msanii huyo alisema kuwa nyimbo zake ambazo tayari amesharekodi mashabiki wake wataziona
muda si mrefu ingawa anawaomba msamaha kwa kuhamia Kenya.

Posted by Bigie on 3:04 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.