UJAZO WA MAJI KATIKA BWAWA LA KIDATU WAONGEZEKA
JAMII 12:14 AM
Msimamizi wa zamu wa Idara ya kuendesha mitambo ya kufua umeme katika mgodi wa Kidatu kwa kutumia kompyuta , Joseph Mwansasu ( wapili kutoka kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( wa kwanza kulia) mfumo wa Teknolojia ya Kompyuta za kuwasha mashine nne za kufua umeme kwenye mgodi wa Kidatu kilingana na mahitaji ya Umeme nchini , Naibu Waziri huyo aliutembelea Mgodi huo Januari 8, mwaka huu, ili kuona hali halisi ya uzalishaji wa umeme na kiwango cha maji kwenye Bwawa la Kidatu.
Kaimu Maneja wa Mgodi wa Kidatu , Joseph Lyaruu , ( mwenye tochi) akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( wa kwanza kulia) kifaa kilichobadirishwa baada ya kufanya kazi muda mrefu na kufanya sehemu nyingi kusagika na maji wakati wa kuzungusha mtambo wa kufua umeme ndani ya mgodi wa Kidatu, Naibu Waziri huyo aliutembelea Mgodi huo Januari 8, mwaka huu , ili kuona hali halisi ya uzalishaji wa umeme na kiwango cha maji kwenye Bwawa la Kidatu.





