Airtel yatoa compyuta na vitabu vya milioni 25/- TZS chuo kikuu cha Dodoma

Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi moja kati ya kompyuta 20 zilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma (UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vina thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya vitabu  vya chuo kikuu vilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma (UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Betty Mkwasa akiongea na waandishi wa habari na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini. Anaefuata ni Makamu mkuu wa chuo hicho profesa idrisa Kikula na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando

Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM)  Profesa Idrisa Kikula (kulia) akiwashukuru Airtel mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  kutoka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini. Kulia ni mkuu wa wa wilaya ya Bhahi Betty Mkwasa na toka shoto ni  Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

======  ======  =====  ======
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote 
vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kwa chuo kikuu cha Dodoma ikiwa ni 
muendelezo wa shughuli zake za kijamii  katika kuchangia sekta ya Elimu

nchini.

Komputa hizo pamoja na vitabu  vimekabidhiwa  kwa Makamu Mkuu wa chuo cha
UDOM kilichopo mkoani Dodoma jana wakati wa hafla fupi iliyofanyika ukumbi

mdogo wa mikutano chuoni hapo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Bhahi Mh,
Betty Mkwasa


Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya wa Bhahi aliishukuru
Airtel Tanzania kutokana na jitihada zake za kushirikiana na serikali 
katika kusaidia sekta mbali mbalimbali ikiwemo elimu 
 “Hili ni tukio muhimu sana mnalofanya Airtel na  inaonesha dhahiri dhamira 
yenu ya kushirikiana na serikali yetu na jamii kwa ujumla  kuchangia elimu 
ili kuinua kiwango cha elimu nchini, hivyo kufanya hivi nchi yetu 
inafaidika sana”


“ninawaomba wanafunzi kuhakikisha mnavitumia kikamilifu kompyuta na vitabu 
hivi ili kujiongezea ujuzi na uelewa zaidi katika masomo kwa manufaa yenu

na  kwa taifa pia”
alimaliza kusema Mh Mkwasa

Nae  Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema”  Airtel chini ya
mpango wetu maaalum wa kuchangia elimu bado tutaendelea kuchangia  elimu

nchini, leo tunaona fahari sana kuweza kujitolea sehemu ya faida yetu pia
kwa taasisi ya elimu ya juu (UDOM),  msaada wetu huu wa kompyta 20 na 
vitabu 104 vya elimu ya juu ni muendelezo wa mpango wetu wa *Airtel Shule 
Yetu *uliodumu kwa zaidi ya miaka saba ukiwa ni maalum kwa kuchangia elimu


 “kwa kupitia mpango wa Airtel Shule yetu  tumeshanikiwa kuzifikia zaidi ya 
shule 800 na kutoa msaada wa vitabu na vifaa vya kufundishia yakiwemo pia

madawati”


Kwa mwaka 2012-2013  bado Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia
sekta ya elimu katika nyanja tofauti ikiwapo; kutoa madawati kwa shule za

msingi na sekondari, kurekebisha majengo ya shule, kutoa computer kwa shule
za sekondari na vyuo lengo hasa likiwa ni kushirikiana na serikali katika 
kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora ili kuweza kupata nguvu kazi 
ya kesho na kulikomboa taifa katika swala la umaskini na elimu duni.


Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM)  Profesa Idrisa Kikula
aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa msaada huo wa kompyuta na vitabu 
umeenda wakati muafaka na unahitajika sana.


“Vitabu na komputa hizi ni muhimu kwa chuo kikuu chetu cha Dodoma, 
tunaamini kabisa vitabu hivi  vitasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba 
wa vitabu na zaidi kuwapatia wanafunzi na walimu nyenzo za kujisomea na

kufundishia pia”
alisema Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM


 “Msaada huu umekuja muda muafaka kwa kuwa Komputa ni muhimu sana kwa elimu  
ya juu ukizingatia karne hii ya sayansi na teknololojia  hivyo zitatumika 
kufundishia masomo mbalimbali ya ICT na kuwapa wanafunzi ujuzi wa

teknolojia ya habari na sayansi ya kompyuta”
alimaliza kwa kusema Profesa
Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM


Chuo kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi
mwaka 2007 huku kikiwa  na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library) kuliko 
chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo hicho

kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku matarajio ni
kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa siku zijazo.

Posted by Bigie on 4:20 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.