Balozi wa Rwanda nchini awasilisha hati ya utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje
JAMII 6:45 AM
Balozi Mteule wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi akiwasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala za hati za utambulisho ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.





