KABURI LA STEVEN KANUMBA LAGEUZWA MRADI


KWELI kufa kufaana, baadhi ya wapigapicha wa kujitegemea jijini Dar wamehamia katika kaburi alilozikwa staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba ‘The Great’ lililopo kwenye makaburi ya Kinondoni kwa lengo la kuwapiga picha watu wanaolizuru kisha kuwatoza fedha.

Tukio hilo lilishuhudiwa na mpekuzi wetu Aprili 13, mwaka huu baada ya kuwakuta wapigapicha hao wakiwapanga foleni waombolezaji na kuwaambia watapigwa picha na wao watatakiwa kulipa fedha ili kuzikomboa.

Mpekuzi wetu alimuuliza mmoja wa wapiga picha hao kiasi wanachotoza kwa kila picha moja ambapo alijibu ni Sh. elfu mbili (2,000).

“Ndiyo utaratibu wetu, mtu yeyote anayetaka kupiga picha kwenye kaburi la Kanumba hata kama atakuja na kamera yake, lazima atulipe elfu mbili,” alisema mpigapicha huyo.

Akaendelea: “Unajua kila mtu ana staili yake ya kumuenzi kipenzi chake pindi anapofariki dunia, sasa kwa sisi tumeona hii ndiyo staili yetu, kwanza tunalilinda kaburi maana kila tunapokuja asubuhi cha kwanza tunafanya usafi ndipo tunaanza kutoa huduma ya kupiga picha kwa dau hilo.”

Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican City Hotel, Sinza jiji Dar.

Posted by Bigie on 2:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.