KUUNGA MKONO MPANGO WA SERIKALI WA KUJENGA BABABARA YA SERENGETI

KUUNGA MKONO MPANGO WA SERIKALI WA KUJENGA BABABARA YA SERENGETI
Waainishwa ALAPA, PINGOs Forum, TAPHGO, NGONET, NYDA, CORDS, TPCF, ni mjumuisho wa asasi za kiraia tunaofanya kazi Tanzania, hasahasa katika ukanda wa Serengeti, na tunafanya kazi hasa katika maeneno ya haki za binadamu na utawala bora.


Tunatoa angalizo kuhusiana na namna ambavyo mradi wa serikali wa ujenzi wa barabara kuu kipitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti umepokelewa ndivyo sivyo.

Mpango wa serikali ya Tanzania kujenga barabara kuu kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti unalenga kuunganisha miji ya Arusha na Musoma na karibu wilaya kumi kwenye ukanda huo. Tunaiunga mkono Serikali kwa mkakati wake wa kujenga barabara kwa ajili ya jamii. Hii ni kwa sababu barabara hii itakuwa na faida kwa jamii zote, na si wananchi wanaoishi Loliondo pekee.
Serikali ya ukoloni ilipotengeneza Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, jamii ziliondolewa kwa nguvu kuelekea Mashariki, na wengine wakapelekwa Magharibi mwa hifadhi. Jamii hizi hazijawahi kulipwa fidia, na mbaya zaidi wanaendelea kuwa katika dimbwi la umaskini.


Taasisi ya ustawi wa wanyama ya nchini Kenya, (ANAW) ilifungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki, kuzuia moja kwa moja serikali ya Tanzania kujenga barabara hii katu, jambo ambalo ni kuwanyima moja kwa moja jamii za Mashariki na Magharibi mwa Serengeti kupata barabara. Baadhi ya taasisi hizi zinafikiria kujiunga na shauri hilo lilifunguliwa kama walalamikiwa.
Tuna imani kwamba Kenya ina agenda zake za siri, kwa kuwa hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara ya nchini humo, ambayo ni njia ya uhamaji ya wanyama, imetawaliwa na hoteli na barabara. Pia kuna miundombinu mingi ya barabara katika hifadhi ya pori kwenye ukanda huu. Kwa mfano, kuna barabara za lami maeneo ya hifadhi ya taifa ya Maasai Mara.

 Barabara ya Nairobi-Mombasa (barabara na reli) zinaigawa Tsavo kuwa mbili; Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi. Licha ya hayo, barabara kuu ya Morogoro-Iringa, inakatiza Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Tunatoa angalizo zaidi kwamba, jamii zinazoishi wilaya ya Arusha, Arumeru, Monduli, Longido, Ngorongoro, Serengeti, Tarime, Bunda, na Musoma, Mashariki na Magharibi mwa Serengeti ambapo barabara imependekezwa kujenga, wana haki ya kuwa na miuondombinu kama jamii zinatajwa kuwa ‘zimestaarabika ’ ulimwenguni kote.

Watu wa Serengeti mashariki na magharibi hawatakiwi kunyimwa barabara katika hali yoyote ile.

Tumesikitishwa sana na tabia ya mashirika ya kigeni na ya ndani ya uhifadhi ya wanyapori kuhadaa ulimwengu kuwa kuna njia mdala ya kupitisha barabara kusini mwa Serengeti. Hiyo siyo njia mbadala.

serengeti_highway.pdf
File Size: 193 kb
File Type: pdf
Download File

Posted by Bigie on 3:47 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.