MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI NA KUZINDUA RIPOTI YA MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA MALARIA TANZANIA BARA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake wakati wa Kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, zilizofanyika leo Aprili 25,2012 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo pia Makamu wa Rais alizindua Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria Tanzania Bara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akikata utepe,kuzindua Ripoti ya Mafanikio ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria kwa upande wa Tanzania Bara, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Malaria Duniani zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Aprili 25,2012. Katikati ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wapili kushoto) ni Kaimu  mkuu wa Wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala, Jordan Lugwimbana. Picha na Muhidin SUfiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia),Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Haji Mponda (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa Ripoti ya Utekelezaji wa Mikakati ya Malaria Tanzania Bara.

Posted by Bigie on 4:44 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.