MUKAMA ATOA MSIMAMO CCM, ADAI KUWA MAFISADI LAZIMA WANG;OKE
JAMII 11:05 PM
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaendelea kuimarika zaidi na kuahidi kuwa wanaotuhumiwa ufisadi lazima watang’oka. Hivyo kimewataka wanachama na wananchi kwa jumla kutokuwa na wasiwasi nacho, kwani kinaendelea kuwa madhubuti.
Kinyume na madai kuwa matatizo yanayoendelea ndani yake yanahatarisha maisha yake, chama hicho kimesema hayo ndiyo yanayokiimarisha na kitakuwa imara zaidi muundo mpya utakapokuwa umekamilika na kuanza kutumika.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), ofisini kwake Lumumba, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Wilson Mukama, alisema muundo huo utaendana pia na tume ya watu 14 itakayokuwa na mamlaka kamili ya kutoa uamuzi, bila kusubiri Kamati Kuu (CC) au Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
“Hivi sasa chama kinajielewa zaidi na kiko imara zaidi ya awali…maeneo yenye mpasuko ni kwa viongozi ambao nao wana sababu zao za kusigana, lakini si kwa wanachama,” alisema Mukama kwa kujiamini.
Alisema kuendelea kuwa na watu ambao machoni mwa jamii wanaonekana hawafai ni kukigharimu chama hicho.
Aliongeza kuwa hata katika uchaguzi mdogo wa Igunga, CCM ilikuwa ikikampeni na mafisadi ambao walikuwa wanaipiga vita, lakini ikafanikiwa kulitwaa jimbo.
Mukama alikiri kuwapo makundi ndani ya chama hicho ambayo yanakitafuna, lakini akasema yote yataondoka tume hiyo itakapoyashughulikia kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, akisema ya sasa itakuwa tofauti kwani ya zamani ilikuwa ya kutoa ushauri bila kuchukua hatua.
Alisema hata wanaokabiliwa na tuhumiwa mbalimbali za kukichafua chama kwa matendo yao, na kutakiwa kujitathmini na kuchukua uamuzi, lakini bado wanang’ang’ania hatimaye watajikuta wameondoka kutokana na muundo huo.
Alifafanua kuwa baada ya uchaguzi wa chama hicho Novemba, kitakuwa chama kipya kilichokamilika ‘kujivua gamba’, kwani mfumo utakaotumika katika uchaguzi huo utakuwa ni wa wajumbe wa NEC kuchaguliwa na wananchi katika ngazi za chini.
“Hivi sasa tunalazimika kubadilisha muundo kwa wajumbe wa NEC mathalan kuchaguliwa ngazi ya kata na wanachama wenyewe, hivyo moja kwa moja, kama mwanachama hakubaliki atachujwa huko huko … hao mafisadi hawatakuwa na nafasi ya kuingia katika uongozi wa chama,” alisema Mukama.
Alisema hata hivyo nalo hilo litasaidia kama kiongozi wa chama hatekelezi wajibu wake vizuri basi atang’olewa na wanachama waliomwingiza madarakani. Kuhusu kumaliza migogoro ndani ya chama hicho, Mukama alisema Kamati ya Wazee wa CCM iliyoundwa itakuwa na jukumu la kukabiliana nayo kwa kuwaita wanaosababisha mvutano na migogoro ndani ya chama.
“Kamati hiyo itaanza kazi kwa kuwaita wanaojipitisha na kutangaza kuwania urais mwaka 2015 na kusababisha mtafaruku ndani ya chama … mpaka sasa sisi hatuna mgombea, lakini muda ukifika mambo yatakuwa hadharani na si hao wanaojipitisha, Kamati itawashughulikia,” alisema Mukama.
Akizungumzia kushindwa kwa CCM katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Arumeru Mashariki, Mukama alisema kulikuwa na masuala mengi zikiwamo kasoro zilizofanywa na wapinzani ambazo zilionekana dhahiri lakini CCM ikatumia uungwana kukubali kushindwa.
Hata hivyo, alisema utakapotokea uchaguzi mwingine, CCM itashinda bila matatizo kwani ilishajua wapi ilijikwaa na nini inatakiwa kufanya.
Wanachama wanaohama Kuhusu wanachama wa CCM pamoja na viongozi kuhama na kujiunga katika vyama vya upinzani, Mukama alisema ni jambo la kawaida ambalo haliwezi kuishitua CCM.
Alitolea mfano wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Arusha, James Millya, kuwa kuondoka kwake si pengo kubwa kwa chama na kwamba kulitarajiwa kutokana na kuchujwa katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Afrika Mashariki.
“Aliona hana mustakabali ndani ya CCM, akaondoka kwania likuwa akitumikia adhabu, hivyo isingekuwa rahisi apitishwe kugombea kwa tiketi ya chama hiki,” alisema Mukama.
Alitumia fursa hiyo pia kukanusha habari kuwa wenyeviti watano wa vitongoji na wanachama 2,402 wilayani Ngorongoro wamekihama chama hicho na kujiunga Chadema kumfuata Millya. “Hawa (Mwananchi) wanaongeza chumvi kwelikweli, taarifa nilizonazo mimi waliohama ni wenyeviti wa vitongoji vitatu na wanachama 200 tu, hao 2,000 wametoka wapi katika eneo hilo la Ngorongoro?” Alihoji Mukama.
Pia alisema hakubaliani na dhana inayoenezwa na wapinzani kwamba vijana wanaikimbia CCM na kuipenda zaidi Chadema, ambapo alisema hata waliojitokeza kuwania ubunge wa Afrika Mashariki wengi walikuwa vijana tena wasomi.
Lakini pia akasema katika kuwajali na kuwathamini vijana, CCM inaandaa mwongozo ambao utakuwa ni kwa ajili ya kusajili vijana kwa utaratibu uliopo na kuwapa uongozi.
“Hata hivi vijiwe vya vijana tunalenga kuhakikisha vinawezeshwa na badala ya kuitwa vijiwe vya kukaa na kucheza tu viwe vya kijasiriamali ambapo vijana watajiunga na kuzalisha,” alisema Mukama.
Mikoa kujitegemea Kuhusu chama kujitegemea, Katibu Mkuu alisema CC imechukua hatua ambapo mikoa imetakiwa kujitegemea badala ya kusubiri ruzuku kutoka makao makuu, na kwa kuanza imeanza na Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, kwa kujilipa mishahara.
“Hizi fedha za ruzuku tunazitumia kwa masuala mengine ya uendeshaji katika chama na kukiimarisha, huko mikoani tumewaagiza wawalipe watendaji wao kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato,” alisema.
“Mikoa ya Ruvuma, Shinyanga, Kilimanjaro, Morogoro na Mbeya nayo tumeanza kuiwekea utaratibu wa kuhakikisha inalipa watendaji wao wote kwa mwaka wa fedha wa 2012/13,” alisema na kuongeza kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha wanachama wanachagua viongozi wanaowataka.
Utendaji wa Serikali Akizungumzia utendaji wa Serikali alisema kama ukidorora, utaathiri chama kwani ndicho chenye Serikali iliyoko madarakani.
“Kama Serikali itatekeleza ahadi zake kikamilifu na hasa kutatua matatizo ya kijamii, ni dhahiri chama kitaonekana kinafanya kazi, kinyume chake kitalalamikiwa tu,” alisema.
Aliongeza kuwa wakulima vijijini mathalan wakipelekewa pembejeo kwa wakati na mazao wanayozalisha yakanunuliwa kwa utaratibu mzuri na kwa wakati, bila shaka hakutakuwa na malalamiko dhidi ya Serikali.
Alibainisha kuwa utendaji mzuri katika kutoa huduma za jamii ndicho kipimo cha msingi cha Serikali kufanya kazi nzuri na kwamba inapaswa kujulikana kuwa chimbuko hasa la matatizo katika jamii ni chakula. “Kama mbinu za kisasa zitatumika kuzalisha chakula kwa wingi mathalan kwa kutumia umwagiliaji, ni wazi hakutakuwa na malalamiko kwa wananchi…upatikanaji chakula ndilo suluhisho,” alisema.
Alisisitiza kwamba mabadiliko ndani ya chama hicho yataendelea kwani kilihitaji ‘upasuaji mkubwa’ ili kuondoa matatizo yaliyopo na si ‘kumeza vidonge’.
Chanzo: Habarileo