“MWANANGU”-SAJNA Feat.VUMILIA
JAMII 7:24 PM
Wimbo huu ulinifikia wiki kadhaa zilizopita.Kwa bahati mbaya na kwa sababu ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa nje ya uwezo wangu,sikupata muda wa kuusikiliza kwa makini na kisha kukupa wewe msomaji na mfuatiliaji wa Mpekuzi nafasi ya kuusikiliza.
Kwa kifupi,si kila wimbo unaotumwa hapa huwa unawekwa moja kwa moja.Hapana.Kuna viwango na kuna utaratibu.
Lazima usikilizwe,wakati mwingine zaidi ya mara tatu na watu tofauti.Ukipita basi huwekwa hewani.Nia ni kusaidia watu watunge nyimbo za maana zaidi kwa maana ya ujumbe na producers waumize vichwa zaidi.
Basi leo muda umepatikana na naomba nikuletee kitu toka kwa Tetemesha Records kutoka kwa msanii wao,Sajna akiwa amemshirikisha msanii mwingine anayekwenda kwa jina Vumilia. Wimbo unaitwa Mwanangu
Huu ni wimbo ambao unazungumzia mapenzi ya mzazi kwa mwanae, na umelenga pande zote yaani mzazi wa kike na mzazi wa kiume, pia mtoto wa kike na mtoto wa kiume.
Lakini pia hata wale ambao hawajapata watoto hawakusahaulika.
Hivyo kwa mantiki hii ni wimbo unaomgusa kila mmoja katika jamii. Usikilize hapa chini na chini tena unaweza kusoma Lyrics za wimbo huo.
Song details
Track Name: MWANANGU
Artists: SAJNA ft. VUMILIA
Lyrics composed by: SAJNA, JOSEFLY & KID BWOY
Arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY & AMBA
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
April 2012
“MWANANGU” Lyrics by SAJNA ft. VUMILIA
Track Name: MWANANGU
Artists: SAJNA ft. VUMILIA
Lyrics composed by: SAJNA, JOSEFLY & KID BWOY
Arranged by: KID BWOY
Produced by: KID BWOY & AMBA
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ
April 2012
Intro:
Mmmmmmh mmh, eeeeh eeh
Oooouuh oooh uuuuh oooh
Chorus
Sijaona kitu kizuri hapa duniani, kama mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Napopata kitu kidogo kikubwa, nakula na mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Verse 1:
Leo watasema madogo, kesho watazua makubwa,
Ujana maji ya moto, umepoa kwa huyu mtoto,
Kweli uanaume ni joto, pale unapokosa mtoto,
Wengi wametenga wake zao kwa kukosa mtoto,
Ufanisi wa jiko ni moto, furaha ya ndoa mtoto,
Nashangaa dada zangu wanaoamua bila hiyana kutupa watoto,
Mtoto wa udongo haoshwi, wa plastiki moto haoti,
Umepewa wa bin-Adam huna budi kusema Asante.
Chorus:
Sijaona kitu kizuri hapa duniani, kama mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Napopata kitu kidogo kikubwa, nakula na mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Verse 2:
Mwanangu kua kua nikutume, ufike kwa mfalme,
Uende kutetea wanyonge, ugumu wa maisha ukome,
Mshike elimu usimuachie,tamaa ujinga zikache,
Wanasema wa mwenzio ni wako, na wewe wangu ni wao,
Kila mmoja mpe heshima, awe na mali asiwe na mali,
Mpe heshimaaa, mpe heshima wewee.
Chorus
Sijaona kitu kizuri hapa duniani, kama mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Napopata kitu kidogo kikubwa, nakula na mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Verse 3:
Ni zawadi ya pekee, niliyopewa mieee,
Ni mtoto wa kike acheni mi niringee,
Aliomnyima ndege utashi na kumpa mbawa arukee,
Ndie aliyenipa mie, mtoto huyu wa kike..
Amenitendea haki nyumbani furaha telee,
Ni mwenyezi Mungu milele ashukuriwe
Bridge
Usikate tamaa, omba na wewe eeeh,
Mungu ni mwema hatoacha chozi lipoteee,
Usivunjike moyo, omba na wewe eeeh
Tena na tena ilimradi usichokeee
Usitupe mtoto si kosa lake yeye,
Mpe malezi bora na elimu aringe baadae,
Alokupa ni mwema wengi wamtafuta yeye,
Uzae japo mmoja ili ndoa itulie.
Bridge
Usikate tamaa, omba na wewe eeeh,
Mungu ni mwema hatoacha chozi lipoteee,
Usivunjike moyo, omba na wewe eeeh
Tena na tena ilimradi usichokeee
Chorus
Sijaona kitu kizuri hapa duniani, kama mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Napopata kitu kidogo kikubwa, nakula na mwanangu,
Yeye damu yangu, mimi baba yake,
Outro
Mwanangu, we mwanangu
Mwanangu, we jembe langu
Mwanangu, we mwanangu,
Mwanangu, wewe jembe langu x2
Oooh oh, Tetemesha
Tete Tetemesha, bwoy bwoy bwoy bwoooooy
Sajna Saj, Sajnaaaaa
End






