MWIMBAJI AMINI ATAJA IDADI YA WASICHANA ALIO WAHI KUWA NAO
JAMII 6:19 PM
Mwimbaji AMINI ambae juzi ametoa video ya single yake mpya ya NI WEWE ameweka wazi upande wake mwingine wa mapenzi sasa hivi baada ya kuachana na LINAH mwaka jana.
Amini amesema “Ilinichukua miezi kama kumi kukaa bila kuwa na mpenzi ambapo mwezi wa kumi na moja ndio nikapata mpenzi mpya, na mpaka sasa uhusiano wangu mpya una miezi michache”
Amini amefunguka zaidi kwamba katika dunia yake ya mapenzi, mwimbaji LINAH SANGA ndio alikua msichana wake wa kwanza, na huyu alienae sasa hivi ni wa pili.
Alipoulizwa kama kupitia kwenye relationships nyingi kuna mfanya aandike vizuri mashairi, Amini alikuwa na haya:
“hapana, naandika nyimbo nzuri kutokana na kipaji changu, marafiki ninao ishi nao pamoja na mafunzo niliyopata THT, kwa hiyo sio mapenzi yanayonifanya niandike nyimbo nzuri”






