MZIMU WA KANUMBA WAMTOKEA BABY MADAHA
JAMII 11:09 PM
MSANII anayefanya vyema kunako gemu la muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha (pichani) amedai kutokewa na mzimu wa Kanumba akimweleza bado hajafa ni maneno ya watu tu.
Akichezesha taya na mpekuzi wetu jijini Dar juzikati, Baby Madaha alisema alitokewa na Kanumba usiku wa Ijumaa iliyopita ambapo walizungumza mambo mengi huku marehemu huyo akimhakikishia kwamba hajafa, “Lakini cha kushangaza alikuwa amejipulizia marashi ya maiti,” alisema Baby Madaha.
Aliendelea kusema kuwa wakati wa maongezi yao walikuwa wamekumbatiana, aliposhtuka alijikuta akitetemeka huku jasho jembamba likimchuruzika.






