Taswira Za Yale Maandamano Ya Wanaharakati Wanaodai Kura ya Maoni Dhidi ya Muungano Zanzibar
JAMII 5:12 PM
Mdau wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muunganoakisindikizwa na polisi kuondoka sehemu ya maandamano
Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza muda mfupi baada ya kushikwa na polisi kwa kufanya maandamano kinyume na sheria
Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza na simu.
Jeshi la Polisi likitoa tahadhari kwa wananchi waliofika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni juu ya Muungano
Kikosi maalum cha Polisi cha kuzuia fujo kikijipanga kukabiliana na wanaharakati waliofika baraza la Wawakilishi
Baadhi ya Wanaharakati waliokuwepo kwenye viwanja vya baraza la wawakilishi wakisubiri hatima yao ya kutaka kuonana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho.





