TETESI: KANUMBA ANA WATOTO KIBAO


PAMOJA na kwamba msanii maarufu, Steven Charles Kanumba amefariki dunia bila ya kujaaliwa mtoto, hali inaonyesha kuwa mambo yanaanza kubadilika kutokana na wanawake kuanza kujitokeza wakidai walizaa naye.

Tayari mwanamke mmoja kutoka Sumbawanga ambaye anaelezwa kuwa aliwahi kufanya kazi ya msaidizi wa ndani kwa Kanumba ameshajitokeza na kutangaza kuzaa na msanii huyo mtoto wa kiume.


Lakini inaelezwa kuna msichana mwingine mkoani Mwanza ambaye ni msomi, tayari ametangaza kuwa na mtoto wa kike aliyezaa na marehemu Kanumba, hali inayoashirikia huenda kuna wengine watajitokeza na kusababishe kuwe na idadi kubwa ya watoto watakaoitwa wa Kanumba.


Huenda kauli ya mama yake Kanumba, Flora Mtegoa kutangaza kuwa anahitaji kuwaona watoto wa mwanaye na kusisitiza wajukuu zake wapelekwe ili awalee inaweza kusababisha wanawake zaidi wajitokeze wakiwa na ‘watoto’ wa Kanumba.


“Nina hofu huenda watoto wakafikia hata kumi, tokea kifo chake haujafika hata mwezi lakini watoto wa Kanumba wanaanza kutangazwa kwa kasi kubwa,” alisema rafiki wa karibu wa Kanumba ambaye ni muigizaji ambaye aliomba kutotajwa.


Pamoja na Mama Kanumba kukaribisha wajukuu zake, ndugu wengine wamegawanyika katika makundi mawili kuhusiana na suala la watoto hao.


Kanumba alifariki usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu na bado chanzo cha kifo chake kina utata kutokana na kuelezwa kilisababishwa na msanii mwingine kina, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye tayari ameshapandishwa kizimbani.

Posted by Bigie on 1:42 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.