AJALI MBAYA JIONI HII: MBUNGE WA ROMBO ANUSURIKA KIFO, MAMA YAKE MZAZI, MAMA MKWE NA MAMA MWINGINE WAFARIKI HAPO HAPO



Mbunge wa Rombo(CHADEMA), Mhe. Joseph Selasini amepata ajali mbaya  sana wakati alipokuwa akiendesha gari lake mkoani Kilimanjaro, ambapo watu 3 kati ya watu 6 waliokuwemo kwenye gari hilo wamepoteza maisha na miili yao imechukuliwa na gari la polisi na  kupelekwa hospitali ya KCMC Moshi kutoka Boma Ng'ombe.
 
 Ajali hiyo imetokea wakati gari alilokuwa akiliendesha kupasuka tairi la mbele na kupinduka eneo la darajani. Taarifa za awali zinasema kuwa watu WATATU kati ya Watano waliokuwemo kwenye gari hilo Wamefariki Dunia hapo hapo - akiwemo Mama yake Mzazi na Shangazi yake!

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro  Absalom Mwakyoma amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo akielezea zaidi amesema
 
ilikuwa ni saa 1:00 jioni maeneo ya Boma Ng;ombe ambapo Mh Joseph Selasini wakati akiendesha gari hilo akitokea Arusha,  ghafla aliona mwendesha Pikipiki wakati akijaribu kumkwepa ndipo gari lake likapinduka.

 Watu wengine akiwemo mbunge huyo na mke wake alifahamika kwa jina la Digna Kavishe waliojeruhiwa katika ajali hiyo, wako katika hospitali ya Boma Ng'ombe  hali zao zinaendelea vizuri na muda mfupi nao watapelekwa katika hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi

Posted by Bigie on 9:52 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.