ASLAY ALITUNGIA WIMBO "JIMAMA" LINALOMTAKA KIMAPENZI


Mwanamuziki wa Bongo Fleva mwenye umri mdogo Aslay amesema amelazimika kumtungia wimbo mwanamke mwenye umri sawa na wa mama yake ambaye humtongoza ili awe mpenzi wake.


Akihojiwa na kituo cha radio cha Capital FM cha Dar es Salaam jana, Aslay mwenye umri wa miaka 16, amesema kusumbuliwa na wanawake wa kila rika wanaomtaka kimapenzi ni jambo linalomkera.

Amesema mwanamke huyo anayeweza kumzaa, humwambia amuite ‘honey’ jambo ambalo humpa woga kutokana na umri wake na kutojua chochote kuhusu mapenzi, kiasi cha kuamua kuandika wimbo huo ili kufikisha ujumbe kwake na kwa wengine wenye nia hiyo.

Aslay ambaye kwa sasa hapendi kuitwa ‘Dogo Aslay, amesema licha ya kuwa mtunzi mzuri wa nyimbo za mapenzi kama alivyoimba kwenye ‘Niwe Nawe” aliomshirikisha Temba, ameongeza kuwa hajafikiria kujihusisha na mapenzi ya vitendo.

Katika mahojiano hayo, Said Fela ambaye alikigundua kipaji chake, amesema aliamua kuanzisha ‘Mkubwa na Wanawe Foundation’ ili kusaidia watoto wenye vipaji vya muziki na sio kwasababu ana fedha.

Katika taasisi hiyo iliyopo Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam, Fela amesema kuna jumla ya wasanii wenye umri mdogo ‘37’ ambao huishi pamoja, na yeye huwasomesha, huwalisha na pia kuwasaidia katika masuala ya muziki.

Fela ndiye aliyehusika pia na kuvumbua kipaji cha mwanamuziki wa kizazi kipya mwenye umri mkubwa kuliko wote Tanzania, Bibi Cheka ambaye shughuli yake ilikuwa ni kuuza mandazi.

Posted by Bigie on 3:31 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.