BREAKING NEWSSS:WANAFUNZI WA MKWAWA IRINGA WAANDAMANA KUDAI MIKOPO YAO
JAMII 7:04 AM
Wanafunzi chuo cha Mkwawa Iringa wakiwa wamepiga kambi nje ya benki ya NMB Iringa kushinikiza kuingiziwa fedha zao .
Wanafunzi wa chuo kikuu cha mkwawa mkoani iringa leo mchana wamefanya maandano na kuzuia barabara ya kuu iendayo IRINGA -Dodoma KATIKA maeneo ya posta.
Wanafunzi hao wamefunga barabara hiyo wakati wakifanya maandamano kutokanana na kucheleweshwa kwa fedha za kujikimu ambazo hutolewa na bodi ya mkopo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi hao wamesema kuwa wameshapeleka malalamiko yao kuanzia ngazi ya chuo hadi kwa mkuu wa mkoa lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Maaandamano hayo yalisambaratika ilipotokea gari ya askari wa kuzuia ghasia na kuwataka wanachuo hao waache kuzuia barabara hiyo kwani barabara hiyo ni huduma ya jamii.
Kutokana na amri hiyo ilibidi waanze kuelekea ofisini kwa mbunge wa Iringa mjini MCH.PETER MSINGWA ambapo mbuge huyo aliwatuliza na kuwaambia wanafunzi hao kuwa na subira kwani kuanzia kesho malipo hayo yatakuwa tayari.
Baaada ya maelezo ya mbunge kuwalizisha wanachuo hao waliamua kurudi chuoni huku wengine wakisema kama mkuu wa chuo hicho hata waambia hatma ya pesa hizo basi leo watakesha ofisini kwake.





