Deo Filikunjombe apewa heshima ya Kifalme Ludewa kwa msimamo wake
JAMII 11:27 AM
Mbunge wa jimbo la Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deo Filikunjombe leo amelakiwa akiwa katika usafiri wa punda baada ya na wananchi wa jimboni kwake na kupewa heshima kutokana na uamuzi wake wa kutia saini katika fomu maalumu Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, chachu iliyoshinikiza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri kufanywa na Rais.
Mhe. Deo (aliyevikwa mataji, aliyevalia shati la kijani na kushikamanisha viganja vya mikono)
Akiwahutubia wananchi, Filikunjombe mbali ya kuwapongeza kwa mapokezi makubwa aliyopata, alisema bado ataendelea kupigania maendeleo ya Wilaya ya Ludewa na Taifa kwa ujumla.
Alisema mjadala katika Bunge liliopita juu ya ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma unaonyesha ni namna gani vitendo vya kifisadi vya viongozi wetu waandamizi vinazuia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010 kama tulivyoahidi kwa watanzania.
“Ndugu wananchi wenzangu, nikiwa mle bungeni, tukiwa tunaijadili ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, inayoonyesha ubadhirifu mkubwa katika fedha za umma; ghafla mawazo yangu yalihama kutoka bungeni yakaja katika vijiji vyetu vya Ludewa, Mavanga, Lusala, Lumbila, na kadhalika. Kitu kama mshale wenye ncha kali wa moto uliuchoma moyo wangu.”
Filikunjombe alisema kuwa alikumbuka mateso makubwa wanayopata wananchi wake na ndio sababu akaumia sana.
“Wakati baadhi ya Mawaziri, wanatumia nafasi zao kujineemesha, nilikumbuka jinsi mwananchi wa Ludewa anavyotaabika kwa miundombinu duni. …nilikumbuka jinsi tulivyo na bara bara mbovu. Nilikumbuka jinsi mwananchi wa Ludewa anavyocheleweshewa kuletewa Pembejeo za Kilimo. Nilikumbuka jinsi mwananchi wa Ludewa anavyoletewa mbegu za kupandia mwezi wa pili wakati msimu wa kupanda mahindi ni mwezi Novemba”alisema
“Nilikumbuka jinsi mawakala wa Pembejeo wanavyokopwa mbolea na serikali yetu, na hakuna kauli maalum inayotolewa. Nikaumia sana…. nilikumbuka namna wanafunzi wa Ludewa wanavyosoma katika mazingira duni, wamekaa chini, walimu hawatoshi, madarasa hayatoshi, nyumba za walimu hazitoshi. Nilikumbuka namna sekondari zetu zinavyokosa maabara. Nilizidi kuumia moyoni mwangu.”
“Kwa niaba yenu ninafarijika kwamba Mhe. Rais ameshaanza kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika. Wito wangu kwake Mheshimiwa Rais ni kwamba asiishie tu kuwawajibisha tu wahusika bali ni lazima pia wafikishwe mahakamani ikiwa ni pamoja na kufilisiwa mali zao walizozipata kwa njia ya kifisadi.”
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinachafuka kwa sababu tu ya kuwakumbatia watu wachache wanaofanya wasiowaaminifu na mafisadi ambao sio Sera ya CCM na wala siyo malengo wala madhumuni kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu.
“Vita tuliyoianzisha ya kukomesha ubadhilifu, wizi, matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ni vita takatifu ambayo kila mmoja wetu anatakiwa kushiriki kwa eneo lake, silaha yetu kubwa ikiwa ni ukweli, haki na ujasiri. Kamwe, msidhani sisi tuliosimama mle bungeni kuwasema wale mawaziri wetu kwamba tunawachukia. Hapana. Bali ukweli ni kwamba kwenye hili ninawapenda zaidi wana Ludewa, na tunalipenda sana Taifa letu kuliko tunavyowapenda wao”.
Nukuu ya habari na picha via francisgodwin.blogspot.com (bofya linki kusoma habari zaidi, na kuona picha nyingine)