Hakuna nia ya kuondoa umaskini - A. Millanga
JAMII 4:31 PM
Ili jambo lolote lifanikiwe duniani linahitaji mambo matatu: nia, sababu na uwezo.
Katika utelezaji likupungua moja kati ya mambo haya huwa hakuna mafanikio. Lakini jambo kubwa zaidi katika haya ni NIA.
Katika misahafu ya Mwenyezi Mungu na mafunzo ya manabii tunausiwa kwamba kila amali ya mja huanza na nia. Hata wahenga wetu wanasema, “Penye nia pana njia.” Katika nia ndipo zilipo fikra na ubunifu, uwajibikaji na uadilifu, kujitolea na kuthamini utu.
Kwa mnasaba na Tanzania na tatizo kubwa la kuongezeka zaidi kwa umaskini - sababu za kuondoa umaskini zipo; uwezo wa kuondoa umaskini upo; lakini nia ya kisiasa na kiuongozi ya kuondoa umaskini haipo. Kila mmoja wetu anafahamu fika kwamba kiini cha umaskini wetu si uvivu wa wananchi kwamba hawataki kufanya kazi kama wengi wa “wataalamu” wenye dhamana wanavyosema.
Kiini ni watawala na watendaji waliojaa ubadhirifu na mabingwa wa ufisadi. Watawala hawa wanadhulumu na kunyonya haki za watu katika taifa letu kwa mori kubwa, motisha kubwa na msukumo kubwa.
Hawana uchungu na nchi. Hawana huruma kwa wajane wanaohangaika kila siku kutafuta riziki za kuwalisha yatima. Hawana

huruma kwa yatima wenye vipaji wanaokosa fursa ya kwenda shule kwa sababu mama hana pesa ya mchango wa dawati. Hawana huruma kwa wanawake wenye mimba wenye uchungu mzito wa kukileta kiumbe kisicho na dhambi diniani lakini wanajifungua wakiwa sakafuni katika mahospitali yetu. Hawana huruma kwa wajawazito wanaonyimwa huduma hadi kufa kwa sababu ya kukosa pesa kuchangia matibabu. Hawana huruma kwa wazee waliotumia nguvu zao za ujana kulijenga taifa lakini sasa hawapati huduma za kuwawezesha kujikimu. Hawana huruma kwa wataalamu wetu ambao taifa liliwasomesha kwa pesa nyingi lakini sasa wameikimbia nchi kwa sababu hawaoni wakitendewa haki. Hawana huruma kwa vijana wanaokosa ajira na nguvu kazi yao kupotea bure bila kuzalisha jambo ambalo linatengeneza kizazi cha watu maskini. Hawana uchungu na raslimali za zinazochotwa tu bwerere kwa kisingizio cha uwekezaji na ukuzaji uchumi.
Uchumi gani huo unaokua bila kukua mifukoni mwa watu?
Maana ya kukua kwa uchumi ni kuinuka kwa hali ya maisha ya watu. Ni uchumi upi mnauongelea? Labda uchumi wa mafisadi maana huo unakuwa kwa kasi zaidi. Tuhabarisheni.Wananchi wanapewa ahadi hewa za kinafiki. Mnafiki akitoa ahadi hatimizi. Akisema anasema uongo. Na ukimwamini anaivunja imani. Inabuniwa mipango mbalimbali ya kiuchumi ambayo malengo yake si kuhudimia umma bali kuuibia na kuumiza umma. Wenye dhamana wanauza raslimali za nchi kwa bei che huku wakimegewa ten pasenti. Hakuna anayewajibishwa. Juu ya hayo ni wafujaji wa kodi ya wakulima na wafanyakazi kwa matumizi makubwa ya anasa kana kwamba hawaujui umaskini uliokithiri unaowazunguka wananchi. Ndugu Agustine Mrema akiwa Mwanza mwaka 2000 katika moja ya mikutano yake hadhara alisema kuwa, “Wanakula kwa mikono miwili tena bila kunawa.” Ulaji huu wa kifisadi unaiangamiza Tanzania.
Katu taifa haliwezi kukusanya mtaji wa kujenga viwanda vipya au kuvifufua viwanda alivyoviacha Mwalimu Nyerere kwa sababu ya wizi wa waziwazi wa watawala na watendaji. Taifa haliwezi kuwekeza katika elimu na utafiti. Baya zaidi hakuna nia ya kudhibiti ufujaji na wizi huu. Wanaachwa tu hivi hivi kwa kisingizio kwamba hakuna ushahidi. Je hata ushahidi wa mazingira haupo? Tunaifahamu mishahara wa mawaziri na watendaji na marupurupu waliyonayo lakini hawawezi kuwa na pesa zaidi ya shilingi bilioni moja katika kipindi cha miaka kumi ya utumishi wao hata kama wanajinyima kiasi gani.
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba miaka miwili iliyopita Waziri Mkuu ndugu Mizengo Pinda alikuwa na ana akiba ya pesa ya shilingi milioni 25. Iangalie historia yake. Zaidi ya nusu ya maisha yake amekuwa serikalini tena katika ‘nafasi nyeti zenye mianya ya ulaji kwa mafisadi’ kisha ulinganishe na wenzake na walio chini yake utapata majibu. Kwa ujanja upi na posho zipi wanazozipata za kumzidi ndugu Pinda?
Hapo bila shaka ushahidi wa mazingira unatupa majibu sahihi kwamba upo ufisadi na dhuluma kubwa inayofanywa na watawala na watendaji wa ngazi mbalimbali serikalini kwa manufaa yao binafsi na si taifa. Hivi kwa nini mali zilizozochumwa kifisadi zisitaifishwe kwa manufaa ya taifa? Kwa nini uozo huu unachwa uendelee kuota mizizi? Nini kinazuia hasa? Sheria? Mfumo? Woga? Kulindana? Fadhila? Jibu li wazi - Nia haipo.
Ukizingalia takwimu za ufisadi unaondelea nchini utaona wazi kwamba Tanzania inao uwezo wa kuondoa umaskini ila pesa inaibiwa. Ukiuangalia uzembe unaofanywa mfano katika suala la umme, msongamano wa magari ya Dar es Salaam, kutotumia treni kama njia kuu ya usafirishaji, kufufua shirika la ndege, viwanda vyetu kutokuzalisha, mikataba mibovu ya madini na uwekezaji utakubaliana nami kwamba Tanzania haipaswi kuwa ombaomba.
Bila nia njema ya kuutumikia umma wa wakulima na wafanyakazi wa Tanzania huwezi kuupunguza umaskini achilia mbali kuuondoa ili hali serikali ina matumizi makubwa ya anasa yanayosababisha mfumuko wa bei unaopaa kila uchao. Bila nia ya dhati huwezi kubuni mikakati ya kuondoa umaskini katika taifa kwa kuzalisha kwa wingi katika kilimo na viwanda. Bila nia nzuri ya kuondoa umaskini huwezi kusimamia vema ukusanyaji kodi na kuondoa misamaha holela ya kodi. Bila nia ya kizalendo huwezi kuondoa umaskini kwa kuendelea kukumbatia ufisadi na uozo. Bila nia yenye huruma huwezi kuondoa umaskini kwa ajira za uchuuzi. Bila nia ya thabiti huwezi kuondoa umaskini bila kutengeneza ajira zenye mafao ya uzeeni.
Wapi utapata pesa za huduma za jamii na mtaji wa kuwekeza katika njia kuu za uchumi? Yote haya yanategemea nia njema ambayo haipo. Nia iliyopo ni wizi wa mali ya umm na ufisadi. Wananchi wakihoji "kulikoni mboja mnafuja mali za umma?" Watawala wanawajibu kwa kejeri na kiburi kwamba "wanawaonea wivu." Wakati umefika sasa tutambue kwamba kuendelea kukua kwa umaskini na kukua kwa ufisadi kunahatarisha amani ya nchi yetu.
Jeshi la vijana wasio na ajira ni kubwa na huwezi kulidhibiti kwa bunduki, risasi na mabomu bali kwa ajira, huduma, matumaini ya maisha bora na ustawi wenye kuonekana katika maisha yao na si kwenye taarifa na takwimu katika makaratasi. Zisuteni nafsi zetu acheni kuiba mali ya umma. Acheni dhuluma na ufisadi, Fanyeni kazi ya kuwatumikia watanzania kwa nia safi yenye uadilifu na uaminifu kwani mliwaomba kura ili muwatumikie na si kuwa watawala dhalimu.
Juu ya hayo muongopeni Mwenyezi Mungu kwani anawalaani kwa kuendeleza ufisadi na udhalimu kwa kula haki za wajane, yatima na maskini. Ni laana iliyoje hiyo ya kulaaniwa na Mfalme wa wafalme na Mwenye uwezo juu ya kila kitu ambaye kukudhalilisheni kwake ni kitu kidogo. Mifano ipo mingi sana ya watawala waliodhalilishwa na Mungu.
Kuweni na utu wenye nia njema.
Ndugu yenu
Amani Millanga "No Choice, No Sacrifice; No Sacrifice, No Access; No Access, No Success.The Choice Should be Guided by the 6Cs of a Good Character: Conscience, Compassion, Consideration, Courage, Control & Confidence."by Amani Millanga
NAAMINI KUWA NAFSI IKITAWALIWA NA TAMAA HATA KAMA INA ELIMU KUBWA NA UTAJIRI KIASI GANI, ELIMU NA UTAJIRI HUO HAVIFANYI KAZI KWA MANUFAA YA WATU