Hawa ndiyo watu tunaowakabidhi ofisi za umma, kisha tunatarajia miujiza
JAMII 4:20 PM
na mijuiza huwa tunaipata kweli, kwa maana yanayoendelea humo maofisini, kama siyo kuogopana na kufichiana siri, sijui!
Unajua fika kabisa huyu aliyekalia kiti hapa ni bumunda zimechukua nafasi ya ubongo kichwani mwake. Lakini kwa kuwa anafahamiana na fulani ambaye ndiye mwenye uwezo wa kushawishi aajiriwe, basi anapewa ajira kwa kujuana.

Si ajabu hata anayemwajiri anajua kabisa hapa ni bomu hili nachukua, ila atafanyaje? Ananusuru mahusiano, basi, nimweke tu labda atabadilika. Ikawa usiku, ikawa asubuhi miaka kadhaa imepita, hakuna maendeleo zaidi ya kufanya kazi kwa mazoea, innovation = zero.
Kosa lako ujitie kiherehere kutaka kulalamika, we! Si vitisho hivyo utakavyopewa bali kufanyiwa vitimbi kila leo. Na tunatarajia kuendelea...! Labda! Huend ipo formula mpya tumeigundua kwa tunayoyafanya ndiyo yatakayotuletea maendeleo.