JINSI JENGO LA YANGA LILIVYOVAMIWA LEO.

.
WATU wanaosadikiwa kutumwa na wapinzani wa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Nchunga wamevamia makao makuu ya klabu, kuvuruga Mkutano wa Mwenyekiti huyo na Waandishi wa habari leo mchana ambapo watu hao wanadaiwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. 


Nchunga aliitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa saa 5:00 asubuhi ya leo, kuelelezea yale yaliyofikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana, Hata hivyo jeshi la polisi lilishusha vikosi vyake hapo na kutuliza vurugu hizo, na hatimaye Nchunga akafanikiwa kuzungumza na waandishi.


Amesema kwa sasa Kamati ya Utendaji inakabidhi jukumu la kiufundi kwa Kamati ya Ufundi na benchi la Ufundi, ikiwemo usajili na uteuzi wa kocha mpya, atakayerithi mikoba ya Mserbia Kostadin Papic aliyetimuliwa.
.

Posted by Bigie on 4:49 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.