JWTZ WAONGEZA NGUVU BAADA YA MAHARAMIA KUWAZIDI POLISI NGUVU KIGOMA.

Kigoma.
Tangu usiku wa May 1 2012 kumekua na taarifa za maharamia kuvamia wavuvi ziwa Tanganyika Kigoma na kupora injini za boti ambapo polisi ilibidi waingilie kati.


Mwandishi Emmanuel Johnson amesema “baada ya polisi kwenda mapambano yalikua magumu hivyo wakarudi kuomba msaada JWTZ ambapo tangu asubuhi walijibizana kwa risasi na maharamia na kupelekea wanajeshi watatu na polisi wawili kujeruhiwa kwa risasi”


Majeruhi wamelazwa kwenye chumba cha upasuaji ndani ya hospitali ya mkoa ya Maweni na mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwenye vyombo vya usalama lakini imeahidiwa kwamba May 3 2012 ndio watatoa taarifa japo hali ya usalama imeripotiwa kuwa nzuri baada ya maharamia kupigwa na kuzamishwa baada ya jitihada za kuwakamata kushindikana.

Tutazidi kukupa kinachoendelea.

Posted by Bigie on 6:08 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.