MADAKTARI WAFURAHIA DR MPONDA NA NKYA KUONDOLEWA

 
CHAMA cha Madaktari  Tanzania (Mat) kimeeleza kufurahishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya, kuwa ametekeleza madai yao.
 
Pia, chama hicho kimesema kimefurahishwa na uteuzi wa Dk Hussein Mwinyi kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa sababu, ni mtendaji anayeaminika.

Katibu Mkuu wa Mat, Dk Rodrick Kabangila, alisema madaktari wamefurahi kuondolewa kwa mawaziri waliokuwapo kwa sababu walikuwa kikwazo kwenye utekelezaji wa madai yao.

“Kwa sasa tuna imani na Serikali, madai yetu na hata yale tunayojadili baina yetu na Serikali yatatekelezwa, tunasema hivyo kwa sababu kama wangeendelea kubaki mawaziri wa awali utekelezaji wake ungekuwa na mashaka,” alisema Dk Kabangila.

Kabangila alisema mawaziri hao walikuwa wagumu wa kutekeleza madai yao na wakati mwingine, walioonekana kuwadharau hali iliyosababisha waingie kwenye mgomo.

“Dk Mwinyi tunamfahamu, wakati madaktari tulipogoma mwaka 2004/05 alikuwa Naibu waziri alikuja kutusikiliza, yapo mambo alichukua hatua kwa wakati,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:

“Akiwa Naibu waziri wakati huo alionyesha tofauti kubwa na Naibu waziri aliyeondolewa Dk Nkya, kwani amekuwa na kiburi hata madaktari walipogoma aliendelea na msimamo wake.”

Kuhusu uteuzi wa mawaziri wapya kwa jumla, Dk Kibangila alisema un
Publish Post
aleta matumaini kwa sababu una sura nyingi mpya na zenye majina yanayoonyesha uadilifu.

Chanzo: Mwananchi

Posted by Bigie on 4:05 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.