MAPOKEZI MAKUBWA YAMSUBIRI FILIKUNJOMBE LUDEWA HII LEO
JAMI 4:31 AM

WANANCHI wa jimbo la Ludewa wameandaa mapokezi makubwa ya kihistoria kwa ajili ya mbunge wao Deo Filikunjombe ambaye wamemfananisha na shujaa katika Taifa wa kupambana na Vitendo vya kifisadi .
Wakizungumzia mapokezi hayo wananchi hao wamesema kuwa wameandaa mapokezi hayo kwa kushirikiana na vyama vyote vya kisiasa Kama njia ya kuunga mkono ujasiri wa mbunge wao Filikunjombe alioonyesha bungeni kwa kuwa mmoja Kati ya wabunge watatu wa CCM walioungana na wabunge wa vyama vya upinzani kusaini fomu ya kutokuwa na Imani na waziri mkuu Mizengo Pinda na kupelekea baraza la mawaziri kuvunjwa .
Mapokezi hayo yamepangwa kufanyika kuanzia majira ya saa 3 asubuhi kwa wananchi hao kutoka pande mbali mbali za jimbo hilo ambao wametumia usafiri wa pikipiki ,baiskeli na malori kufika eneo hilo la Magereza kwa ajili ya kumpokea mbunge huyo anayetokea jijini D'Salaam .
Mbunge Filikunjombe ameendelea kujizolea umaaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake ya kupinga Vitendo vya kifisadi jambo linalomfanya kuwa ni kada na mbunge wa CCM mpambanaji .
Mtandao huu ututakuwezesha kupata matukio hayo ya mapokezi ya mbunge huyo. Chanzo: www.francisgodwin.blogspot.com