Mawaziri Wa Fedha Watoa Maelezo

 Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha mara baada ya kubadilishana hati ya mkataba wa mkopo nafuu na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Waarabu inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) Bw. Abdelaziz Khelef (kulia) wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1 kutoka Wete hadi Chakechake kisiwani Pemba. Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 15.
Waziri wa Fedha na Mipango Ofisi ya Rais Yusuf Omar Mzee (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Arusha juu ya umuhimu wa barabara mpya inayotarajiwa kujengwa kutoka ChakeChake hadi Wete kisiwani Pemba mara baada ya Tanzania na  Benki ya Waarabu inayojishughulisha na Maendeleo ya Uchumi ya Afrika (BADEA) kusaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 22.1. Kulia ni Waziri wa Miundombinu ,Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Zanzibar Hamad Masoud  

Picha na Hazina- Arusha.

Posted by Bigie on 2:18 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.