Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi kujitenga na Morocco
habari za kitaifa, JAMII 10:51 AM
Bernard Membe (Mb) akizungumza na wanhabari jijini Dar es Salaam leo (photo: marygorethrichard.blogspot.com)
Tanzania imetangaza msimamo wake kuhusu kuitambua nchi ya Sahara Magharibi na kutaka iwe Jamhuri huru inayojitawala ana kujitegemea, licha ya kuwepo kwa upinzani mkali kutoka kwa nchi ya Morocco ambayo ndiyo inayoitawala nchi hiyo kwa sasa.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema mazungumzo yanaendelea baina ya Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Morocco ili kuiwezsesha Sahara Magharibi kukwa huru, ambapo imetawaliwa an Morocco kwa zaidi ya miaka 30.
Umoja wa Mataifa umependekeza kura za maoni zipigwe ili kuamua ikiwa wananchi wanataka kujitawala au kuendelea kutawaliwa, lakini Morocco imepinga pendekezo hilo.
Bofya kifute cha pleya kusikia sehemu ya kauli ya Membe.

Yatokanayo na taarifa hii
Yamenikumbusha harakati za Wanauamsho Zanzibar na baadhi ya Watanzania kuhusu suala la Zanzibar kujiengua kutoka katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sina shaka wala tashwishi yoyote kwamba atatokea mtu kunifahamisha kuwa "haya ni masuala mawili tofauti" na nisipende kulinganisha mambo, kwamba moja inahusu nchi "kutawaliwa" wakati kwenye nyingine inahusu nchi zilizopo kwenye "muungano halali" zinazotaka kujitenga.
Naam, "sawa" kuungana kama Marekani na "sawa" kujitenga kwa Northern Ireland kutoka The United Kingdom na "sawa" kujirenga Biafra... ila si sawa hata kuzungumzia masuala yanayowatatiza Wazanzibari na Watanzania waliopo kwenye Muungano.