SIKU YA WAUGUZI DUNIANI YAFANA WILAYANI RUNGWE
JAMII 5:08 AM
Wauguzi wa wilaya ya Rungwe wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya wauguzi duniani |
| Mgeni rasmi mkurugenzi wa wilaya ya Rungwe Noel Mahyenga aliyeshika taa akiongoza maandamano hayo |
| Mkurugenzi wa wilaya Rungwe akiwa na muuguzi mkuu wa wilaya Sophia Mkonongo wakiwa wameshililia mishumaa kama ishara ya upendo |
| Mkurugenzi wa wilaya akitoa zawadi kwa mmoja ya wagonjwa kuonyesha upendo kwao |
Wauguzi nchini wametakiwa kuwa na moyo wa upendo na kuwajari wagonjwa wawapo kazini kwa kuwa muuguzi ndio mtu anayetoa huduma kwa ukaribu na muda mwingi kuwa na Mgonjwa. Akiongea na wauguzi mkurugenzi wa wilaya ya rungwe Noel Mahyenga katika siku ya wauguzi Duniani amewataka kuongeza huduma kwa kuwa jari na kutoa huduma inayomstahiri mgonjwa. Naye muuguzi mkuu wa wilaya ya Rungwe Sophia Mkonongo ameita serikali kutatua baadha ya changamoto amazo sasa imekuwa ni kero katika fani ya uuguzi. |





