SIRI YA NDOA YA SKAINA KUVUNJIKA SIKU 4 BAADA YA KUFUNGWA YATHIBITIKA
JAMII 12:08 AM
Hivi karibuni msanii huyo aliyeolewa na mwanaume aitwaye Saad Omary, kujifungua kwake mtoto wa kike ni kupaka rangi yale madai ya awali kwamba aliachika baada ya mumewe kugundua ana ujauzito usiomuhusu.
Awali, Skaina alipokuwa akizungumzia sababu za ndoa yake kuvunjika alijiteteta kwa kusema aligundua Saad alikuwa tapeli kwa vile alimkimbia wakiwa kwenye fungate.
TUNAMNUKUU MADAI YA AWALI:
“Ndoa imevunjika mume wangu (Saad) alinikimbia tukiwa kwenye fungate, aliniaga anakwenda Uholanzi kikazi, nikarudi kwetu kwanza kwa ahadi kuwa tutaendelea kuwasiliana.
“Cha ajabu nilikaa nyumbani kwa muda mrefu, nilipomtafuta kwenye simu kuna wakati anapokea na kunijibu ovyo, hivyo nikaamua kudai talaka yangu.”
MADAI YA MSINGI
Hata hivyo, utetezi wake huo ulizimwa kwa kishindo na maelezo ya rafiki wa karibu wa Saad kuwa wakati wanandoa hao wakiwa kwenye fungate mwanaume aligundua mkewe huyo ana ‘kibendi’ cha mwanaume mwingine lakini alifanya kuwa siri pengine ili ‘ambambike’.
“Nyie mlikuwa hamjui lakini ukweli ni kwamba wakati wakiwa fungate, Saad alimsaula viwalo Skaina kwa lengo la ‘kuburudika’, ndipo akabaini tatizo, akaona umuache lakini siyo kweli kuwa mwanaume alikuwa tapeli.”
Skaina alijifungua Mei 2 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan iliyopo mjini Iringa.
MAHESABU YA HARAKA
Kujifungua kwake Mei, 2012 kunaleta picha kuwa wakati msanii huyo alipofunga ndoa (Oktoba 7, 2011) alikuwa na ujauzito wa miezi miwili.
Kwa maana hiyo, madai ya mumewe ambaye aliamua kumuacha yalikuwa ya kweli kuliko utetezi wa msanii huyo.






