WAWAKILISHI WA BONGO BBA HAWA HAPA


Wawakilishi wa Tanzania ndani ya Big Brother ‘StarGame’ 2012, Julio na Hilda.


KITENDAWILI cha nani anaiwakilisha Tanzania kwenye kinyang’anyiro cha Big Brother ‘StarGame’ 2012, Jumapili iliyopita kiliteguliwa baada ya kutangazwa majina ya washiriki wawili, ‘mapatna’ Julio na Hilda.

JULIO
Julio Batalia ni Mtanzania, mkazi wa Dar es Salaam, mwenye umri wa miaka 27, akiwa na Shahada ya Uzamili katika mambo ya mahesabu. 


Kwa mujibu wa Julio, alifikia hatua ya kuingia kwenye Big Brother StarGame kutokana na aina ya maisha yake na baada ya rafiki yake kipenzi, Hilda kuwa mmoja wa washiriki anayeamini atakuwa bora zaidi.


Julio alisema Hilda ni mrembo mwenye maisha halisi na siyo ya kuigiza hivyo huwa anapenda kuwa karibu naye muda wote.
“Yuko smati, anavutia sana, Afrika nzima itampenda mno,” alisema Julio akimzungumzia Hilda.


HILDA
Hilda ni Mtanzania, mkazi wa Morogoro mwenye umri wa miaka 28 akiwa ni mfanyabiashara mwenye mtoto mmoja wa kiume ambaye alivutiwa na Biggie mwenyewe (kaka mkubwa) kuingia Big Brother StarGame.


“Anaonekana ni mtu mwenye changamoto ndani ya mjengo hivyo nilijisikia furaha sana nilipochaguliwa kuungana naye kwani nataka changamoto zake,” alisema Hilda na kuongeza:


“Julio ni swahiba wangu mkubwa. Ni mtu mchangamfu, mzuri na mwelewa.”

Kwa mujibu wa Hilda, fedha watakazoshinda, yaani dola za Kimarekani 300,000 (takribani Sh. milioni 500) baada ya kukaa mjengoni kwa siku 91, watazitumia kusaidia makundi mbalimbali ya wasiojiweza kwenye jamii.


Washiriki hao wa Bongo, Julio na Hilda na wale wa Zimbabwe, Maneta na Teclar, tayari wamewekwa kwenye mstari mwekundu wa kuoneshwa mlango wa kutokea Jumapili ijayo hivyo kitakachowaokoa ni wapiga kura kupitia mtandao wa Big Brother Africa.

Posted by Bigie on 12:41 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.