MISS EAST AFRICA 2012 SUDAN



Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012 amepatikana.

Mrembo huyo ni Miss Akuot Philip Suzan (20) mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa
Juba, Sudan ni mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele Nchini Uganda mwaka huu.

Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.

Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius,Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.

Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu
wa Africa.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na
Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini
Dar es salaam, Tanzania.

John Bukuku

Posted by Bigie on 1:52 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.