ALICHOSEMA NAIBU WAZIRI KUHUSU HASARA YA AJALI YA NDEGE YA AIR TANZANIA KIGOMA.

Kwenye kipindi cha maswali na majibu Aug 1 2012 bungeni Naibu waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba alijibu kuhusu hasara ya ajali ya ndege ya shirika la ndege Tanzania iliyotokea Kigoma tarehe 9 April 2012 pamoja na uhaba wa ndege kwa sababu shirika la ndege Tanzania linazo ndege mbili tu.


Tizeba amesema “ni kweli kwa sasa shirika la Ndege Tanzania linazo ndege mbili tu, moja ikiwa inamilikiwa na shirika lenyewe na nyingine ya kukodi, historia ya hili shirika nadhani inafahamika kwa sababu baada ya kuingia ubia wa aina mbalimbali huduma zilidorora na likaserereka kuelekea huko”

.Kuhusu hasara iliyojitokeza kwenye ajali Kigoma, Naibu Tizeba amesema “ndege inayo gharama yake na ndio maana baada ya kupata ile ajali tulilipwa bima kiasi cha shilingi bilioni 10.2 lakini hasara iliyopatikana ilikua kwenye biashara hasaa na sio gharama ya ndege yenyewe.

Gharama iliyopatikana kutokana na kulazimika kuwalipia hoteli abiria walioshindwa kusafiri kutokana na ajali hiyo imetajwa kwamba ni milioni 499 ambayo ilitumika kulipia hoteli pamoja na mambo mengine.

Tayari imetangazwa na waziri wa Uchukuzi kwamba pesa hiyo ya bima itatumika kununua ndege mbili mpya.

Hii ndio ndege mpya iliyokodiwa na shirika la ndege ATC.
Ya kukodi.

Posted by Bigie on 2:29 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.