"NEY WA MITEGO ATAKUFA KWA KUCHOMWA KISU AU KUPIGWA RISASI"....HUU NI UTABIRI WA MCHUNGAJI



Mtu anayejiita mchungaji hivi karibuni amemtabiria kifo rapper Ney wa Mitego kwa kudai kuwa atafariki kwa kuchomwa na kisu au kupigwa risasi.

Ney amesema mchungaji huyo alimfuata nyumbani kwake na mpaka picha zake anazo.

“Nilimrekodi pia, alikuwa anaongea kwa confidence sana, lakini mimi sitishiki na wala siogopi, mimi namtegemea mwenyezi Mungu. Hiki ninachokifanya ni kipaji cha pekee na hawajui kwanini najiamini na siwezi kuacha kukifanya hiki,” Ney alikaririwa jana Jumamosi kwenye kipindi cha Tagz Weekly cha DTV.

Ney amesema mtu huyo alimwambia kuwa ameoneshwa na mwenyezi Mungu, kwamba yeye ni nabii na ni lazika amfikishie ujumbe huo.

“Mwanzo alifika home, aliwakuta wadogo zangu, mimi nikasema amekuja from nowhere siwezi kuongea naye, alianza kuongea na madogo, akawaambia anataka kuonana na Ney mwenyewe, nikawaambia mwambie aondoke. 

Nikaona haina haja kwanini nisionge naye, aliacha namba za simu, dogo akampigia akarudi, kurudi ndio akaongea aliyokuwa anaongea.” 

”Watanzania wajue kuwa wameanza kutokea watu ambao wanatabiri kifo changu ila nawaambia mimi najua siku yangu ya kufa labda wao waendelee kufanya harakati zao ili kunifelisha na hawawezi kunifelisha, mwenyezi Mungu ndio anajua mimi nafanya nini na wapi ambapo ntaishia.”

“Nilishawaahidi watanzania kwamba huu ni muziki wangu na hii ndio hip hop na hizi ndio harakati ambazo natakiwa kuzifanya,”aliongeza.

Pia amesema siku za hivi karibuni amekuwa akipokea meseji za vitisho kutoka kwa watu wanaomtishia kumuua.

Posted by Bigie on 12:09 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.