BINTI WA MIAKA 16 NCHINI ZIMBABWE ASIMULIA ALIVYOJIUNGA NA DINI YA KISHETANI


Mtandao maarufu wa Naija Gists umeripoti kwamba binti mmoja wa miaka 16 Zimbabwe ameshtua nchi baada ya kujitokeza na kusema yuko kwenye dini ya kishetani ambayo waumini wake hunywa damu za watu.

Kilichowashtua wengi zaidi ni kwamba amewataja watu 38 ambao wamefariki tayari ,na hiyo ni kutokana na kunyonywa damu na waumini wa dini hiyo.

Hakuishia hapo, huyu binti ametaja mpaka majina ya watu 60 anaoshirikiana nao kwenye hiyo biashara akiwemo mchungaji wa kanisa moja maarufu lililopo cawdray park Bulawayo na ametaja mpaka nyumba ilipo na kuadai kwamba kwenye hiyo nyumba kuna chumba cha chini ya ardhi ambacho ndio watu huwa wanawekwa huko wakisubiri kuuliwa damu ipatikane.
.
Alijiunga na hiyo dini akiwa na umri wa miaka 15 tu na ilikua ni baada ya kushawishiwa na mwanaume ambae alikua ni mpenzi wake mwenye umri wa miaka 32, siku moja akiwa kwenye kituo cha basi na boyfriend wake, alijisikia vibaya mwilini na akakaribia kuanguka ndio boyfriend wake na rafiki zake wakamnyanyua na kumpeleka kwenye nyumba iliyopo karibu na kituo cha basi.

Kwenye hiyo nyumba ndio kuna hicho chumba cha ardhini ambapo alilishwa damu ya watu, polisi wa Zimbabwe wamethibitisha kupata hizo taarifa toka wiki iliyopita ila hawajasema chochote mpaka  wakimaliza uchunguzi.

Posted by Bigie on 11:12 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.