BONGO MOVIE IMENIFANYA NIONEKANE CHANGUDOA"....AUNT LULU


MSANII wa filamu na ambaye pia aliwahi kuwa mtangazaji wa TV Aunty Lulu, amesema kuwa anajuta ni kwa nini alishawishika kuigia kwenye tasnia hiyo ya filamu kwani ni bora angeendelea na kazi yake ya awali, kwani huko kumemfanya aonekane kama changundoa wakati hayuko hivyo.

Tasnia ya filamu imekuwa ikiwaharibu vijana wengi hasa wakike wanaopenda kufanya kazi hiyo na mwisho wa siku wanaonekana kama wamepoteza muelekeo wa maisha, kutokana na anasa zilizopo ndani ya tasnia hiyo.

Aunty alisema kuwa awali kabisa alipenda kufanya kazi hiyo lakini kadri siku zinavyokwenda mbele anajiona wazi kuwa amebandilika na amekauwa na tabia chafu ambazo hazina mfano.

Alidai kuwa inawezekana hakujua namna ya kujipanga pindi alipokuwa anaigia kwenye tasnia hiyo, lakini sasa anaona wazi kuwa tayari ameshazama kwenye shimo na kutokana kwake ni vigumu kwani hayo ya sasa ndiyo maisha aliyozoea.

“Awali sikuwa hivi asa sijui hii ni kwa sababu ya kuingia kwenye filamu au vipi, lakini kuna matukio mengine nimeyafanya ambayo kwa kweli si mfano wa kuigwa,” alisema.


Dtalk

Posted by Bigie on 1:56 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.