BREAKING NEWS: SAJUKI WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA



Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India
 
MSANII nyota wa filamu Tanzania, Juma Kilowoko, ‘Sajuki,’ amefariki dunia saa moja asubuhi ya leo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

Sajuki aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba 2012, alikofikishwa akitokea Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya kuanguka jukwaani jijini Arusha, alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake ikiwa ni harakati za kutafuta fedha michango ya pesa za kumpeleka tena India kupata matibabu.

Katibu wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate nafuu ili Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India.

Makubi alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na wadau kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na msanii huyo kwa ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya mazishio yake.

Kabla na baada ya kuifika India kwa matibabu, Sajuki aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini, ambapo aliporejea alionekana kuimarika kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.

Kifo cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii nguli wa filamu na muziki ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven Kanumba, John Maganga, Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ walifariki kwa nyakati tofauti kutokana na maradhi na ajali.
 
Mchakato wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar es Salaam. 
 
MUNGU ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen.

Posted by Bigie on 9:26 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.