CHADEMA YAFUNGUKA KUHUSU KAULI ZA NAPE NNAUYE KWAMBA KIKO MBIONI KUVUNIKA KWA "UBAGUZI"


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimesema kuwa kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, NAPE NNAUYE, kuwa chama hicho kitakufa kutokana na kuwa na Sumu ya Ubaguzi, haina ukweli wowote, na kumtaka kiongozi huyo kutafakari zaidi kauli hiyo kwa maslahi ya Chama chake.
 
Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo wa CHADEMA, BENSON KIGAILA, amesema CHADEMA hakiwezi kufa kwa dhana iliyozungumzwa na NAPE, na badala yake Chama hicho Tawala ndicho kinachoweza kufa kutokana na kukabiliwa, na changamoto nyingi ikiwemo ufisadi.

 
Katika Hatua nyingine CHADEMA kimemtaka Naibu Katibu wa CCM, MWIGULU NCHEMBA, kutoa ushahidi wa kauli aliyoitoa hivi karibuni, kuwa Chama hicho kimekuwa kikipanga mipango ya mauaji na kubanisha kuwa kauli hiyo, imelenga kulidhalilisha jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa

Posted by Bigie on 12:23 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.