CHAMELEONI NDANI YA MTEGO MZITO.....YAWEZEKANA AKASHITAKIWA KWA KOSA LA MAUAJI
habari za kitaifa, JOSE CHAMELEONE 12:59 AM
Mwanamuziki wa Uganda , Jose Chameleone anaweza kujikuta akikabiliwa na kesi ya mauaji kutokana na kifo cha kijana mwenye miaka 27, Robert Karamagi aliyefariki hospitali baada ya kujichoma moto nyumbani kwa mwanamuziki huyo.
Joseph Mayanja na mke wake Daniella Atim Mayanja na wengine wanaoishi nyumbani kwake wanafikiriwa na polisi kuhusu kushtakiwa kwa kifo Karamagi.
Ripoti za awali zinadai kuwa Karamagi alijaribu kupora nyumbani kwa Chameleone lakini alikuwa na nia ya kumuua Daniella. Hata hivyo kwa bahati mbaya alijichoma moto mwenyewe uliomsababishia majeraha na hatimaye kifo.
Daniela (mke wa Chameleone)






