MENEJA WA KUNDI LA ‘PAH ONE’ AKANUSHA KUSAMBARATIKA KWA KUNDI HILO


WAKATI kukiwa na tetesi kuwa lile kundi la muziki wa bongo fleva Pah One, limevunjika meneja wa kundi hilo amekana ishu hiyo na kudai kuwa kundi bado lipo lakini kikubwa ambacho kilitokea ni kutokuelewana ndipo baadhi ya wasanii walipoamua kusafiri na kubaki wawili na watakaporejea wataendelea kama kawaida.
Kundi hilo linaundwa na vijana wanne ambao ni Nahreel , Ola, Aika na Igwee ambao wamekuwa wakifanya muziki wa tofauti ambao unaweza kuwatambulisha zaidi hata kimataifa.

Hata hivyo meneja huyo alipotakiwa kujitambulisha jina lake alidai huwa hapendi jina lake litokee kwenye vyombo vya habari na kitu anachokifanya yenye ni kuwasaidia vijana.

Posted by Bigie on 2:28 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.