PROFESA JAY AMPA SHAVU VANESSA MDEE....ADAI KUWA KIPAJI CHAKE HAKINA MPINZANI



Tangu aachie wimbo wake wa kwanza, Closer, Vanessa Mdee amekuwa akimwagiwa sifa kibao kutoka kwa watu mbalimbali kiasi ambacho kimewafanya baadhi ya watu wahisi kama anapendelewa. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa mtangazaji huyu ameendelea kujipatia mashabiki kibao. 



Shabiki wake mpya wa sasa ni heavy weight mc, Joseph Haule aka Profesa Jay.Profesa Jay ameshindwa kujizuia na leo kwenye mtandao wa Twitter amefunguka kwa Vanessa kwa kutweet, “ Vanessa Mdee una kipaji cha hali ya juu sana, nakuomba sana sana ukichukulie SERIOUS, maana nahisi kama bado unauchukulia MUZIKI kama HOBBY!”

“Coming from you. That means everything. Nashukuru, na nimekusikia. I’m serious about this thing. Asante,” alijibu Vanessa.

Naye Dj maarufu wa nchini Marekani ambaye hivi karibuni alikuja nchini, Dj Topsin alitweet kuusifia wimbo wake kwa kuandika, “Ayo @VanessaMdee, ‘Closer’ is crackin’. I’m feelin’ flavor overall & the usage of both languages. #WorldWideReach #SeeYouAtTheTOP.”

Hizi ni tweets zingine za radio na madj kutoka Rwanda na Kenya zinazousifia wimbo huo:

@Fifilyn: Tune in Kigali to Radio 10 for @VanessaMdee #CLOSER!!!! CHUUUUNNNEEEEE big up girl!!!

@xclusivedeejay: Kenyan djz look for closer by @VanessaMdee certified jam across borderz!!!I’ll be droppin it tonight at bacchus lounge…heavy tune.

Posted by Bigie on 1:46 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.