WAZIRI MKUU MSTAAFU, EDWARD LOWASSA ANUSURIKA KUFA KATIKA AJARI


 Gari la  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali iliyotokea jana asubuhi.
-- 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa Mh. Edward Lowassa amenusurika kifo,baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.

Gari hilo la Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa liligongwa na basi la Morobest, wakati basi hilo lilipolipita basi jingine kwenye daraja na kukutana uso kwa uso na gari lakini dereva wa  Mh. Lowasa kwa ustadi mkubwa alilikwepesha gari lisigonge upande alipokuwa amekaa  mzee na kuligonga ubavuni nyuma kwa upande wa dereva na hakuna aliyejeruhiwa.


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa na msafara wake aliendelea na safari hadi morogoro ambako ameshiriki katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Kilakala ambapo yeye na Marafiki Zake Wamechangia Shilingi Milioni 18

Posted by Bigie on 6:31 PM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.