H BABA AMZIBA MDOMO FROLA MVUNGI....."ACHANA NA SHILOLE MKE WANGU"


MSANII wa miondoko ya bongo fleva H.Baba ameamua kufunguka juu ya malumbano yaliyotokea kwa wasanii wawili wa filamu nchini Shilole na Frola Mvungi,na kuelezea hatua ambazo amezichukua kuhusu malumbano hayo

Akiongea na safu Maisha H.Baba alisema kuwa hatua ambayo ameichukua ni kumshauri mkewake mtarajiwa Flora Mvungi kuachana na malumbano na kuendelea na kazi zake kwani wanamajukumu mazito yanayowakabili

Alisema kuwa ameamua kumshauri hivyo  kwa sababu tabia ya mke wake na malumbano ni vitu ambavyo haviendani naye na kutokana na majukumu na heshima ambayo anayo kwa jamii hapaswi kufanya hayo

"Unajua mke wangu hapaswi kurumbana rumbana hovyo kutokana na hadhi yake ambayo anayo kwa jamii hivyo kwa sasa lazima anisikilize mimi nilichomshauri na kutulia ili mambo mengine yaendelee"

Frola anajiandaa kutoa single nyingine hivi karibuni ambapo jina la nyimbo hiyo halijawekwa wazi

Posted by Bigie on 10:23 PM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.