"VUMILIA MWENZANGU....NI IMANI YANGU KUWA KAJALA ATAACHIWA HURU"....MAMA LULU AKIMFARIJI MAMA KAJALA


BAADA ya mwanaye kutoka mahabusu kwa dhamana, mama wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, hivi karibuni alinaswa akimpa mbinu mama wa msanii Kajala Masanja zitakazomsaidia kumuokoa mwanaye. 

Akina mama hao walinaswa na mwandishi wetu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Kajala na mumewe, Faraja Chambo walifikishwa kwa ajili ya kujitetea kwenye kesi inayowakabili ya kutakatisha fedha haramu.


Katika tukio hilo, mama Lulu ndiye aliyeanza kufika mahakamani hapo na baada ya muda, alitokea mama Kajala ambapo walisimama pembeni na watu waliokuwa karibu yao walidai mama Lulu alikuwa akimpa mwenzake mbinu za kumwezesha kumuokoa mwanaye na kesi hiyo.


“Naona mama Lulu anampa mwenzake mbinu za kumuokoa Kajala ila amefanya la maana sana kuja kumpa kampani na kwa uzoefu wake wa mahakamani anaweza kumsaidia,” alidai mama mmoja aliyekuwa karibu yao.


Hata hivyo, wazazi hao walisitisha mazungumzo baada ya Kajala na mumewe kutolewa chumba cha mahabusu na kupandishwa kizimbani ambapo Wakili wa Serikali, Renald Swai aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 (kesho) baada ya kupokea udhuru kutoka kwa hakimu aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo, Sundi Fimbo.


Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mama Lulu aliendelea kuwa karibu na mama Kajala ila kilichowatawanyisha kilikuwa ni mwanga wa kamera .

Posted by Bigie on 1:44 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.