CHAKUA YAPANIA KUIBURUZA MAHAKAMANI SUMATRA BAADA YA KUPANDISHA NAULI ZA MABASI NA DALA DALA KIHOLELA


Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimesema kinaiburuza kortini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (SUMATRA), kwa madai kuwa hakikushirikishwa kwenye mchakato wa kuongeza nauli za abiria.
Aidha, CHAKUA kimeitaka serikali kuuwajibisha uongozi wa juu wa SUMATRA kwa kuifuta na kuunda upya kwa madai kwamba imeshindwa kusimamia maslahi ya wananchi wanyonge.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mshauri wa chama hicho, Wilson Mashaka, alisema tangazo la kupandisha nauli halikujengwa kwa dhana ya ushirikishwaji, kwani vikao vilivyofanyika kati ya Septemba na Novemba, 2012, vilifanyika kwa kuwashirikisha wamiliki wa mabasi lakini wadau muhimu kama CHAKUA hawakushirikishwa.

Posted by Bigie on 2:28 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0
.

Featured Post

NEC ya ahirisha uandikishaji kwa BVR mikoa 4 nchini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji kwa BVR katika mikoa minne  ambayo ni  Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja ...

2010 BlogNews Magazine. All Rights Reserved. - Provided by Free Blogger template.